Ni wikendi iliyosheheni mambo mengi ila lilosifika zaidi ni hafla ya Kikwetu Night iliyofanyika katika ukumbi wa Bakulutu siku ya Jumamosi.
Ni usiku uliokuwa wa kukata na shoka kwa mashabiki wa Bango kutoka kwa bendi tofauti zilizoungana kwa ajili ya tamasha hilo.
Kando na kupata burudani babkubwa mashabiki wa Radio Kaya walipata fursa ya kipekee ya kuungana na watangazaji tajika katika hafla hiyo.
Wakiongozwa na mwendeshaji kipindi cha Misakato Ya Bango, Dominick Mwambui, Watangazaji Beatrice Dama na Kalambua wanaoendesha kipindi cha VoroniEnehu na Chikoyokoyo anayeendesha kipindi cha ChikaChika walijumuika na mashabiki wao.
“Napenda sana Radio Kaya na hafla hii imefana kuliko za stesheni zengine wikendi hii,” alisema Joan Umazi mmoja wa mashabiki waliojitokeza katika hafla hiyo.
Kando na shabiki huyo wasanii waliofika katika hafla hiyo pia waliisifia sana hafla hiyo.
Siku hiyo pia ilikuwa siku ya uzinduzi rasmi wa bendi mpya ya Bango ijulikanayo kama New AfricanSound, itakayojumuisha James Ngala na Julius Mwenyewe.
the “MWENYEWE”title is for mzee NGALA PEKEAKE