Story by Mwahoka Mtsumi –
Radio Kaya imeshinda Tuzo za Kuza Broadcasting Awards mwaka wa 2021 kama stesheni bora zaidi kanda ya Pwani.
Hafla hiyo ya kutangazwa kwa tuzo hizo imeandaliwa na Malmlaka ya mawasiliano nchini CA jijini Nairobi na Radio Kaya ikatangazwa stesheni bora zaidi kanda ya Pwani.
Radio Kaya imetambulika kama kituo cha habari kinachoangazia taarifa tendeti, makala yaliosheheni jumbe za kuielimisha jamii, vipindi vinavyoangazia maswala ya jamii na stesheni inayoangazia maswala ya kitamaduni.
Hata hivyo watangazaji wa Radio kaya wamefurahia ushindi huo na kuwapongeza wasikilizaji wa kituo cha habari za Radio Kaya kwa kushirikiana na Wanahabari wa Radio Kaya.
Congratulations