Picha kwa hisani –
Wakaazi wa Kaunti ya Mombasa wamehimizwa kujitokeza na kuchangisha damu kwa hiari ili kuokoa maisha.
Shirika la Vijana la Redsplash linaloongoza kampeni ya kukusanya damu ,limesema hospitali nyingi za umma kanda ya Pwani zinakabiliwa na uhaba wa damu akitoa wito kwa wakaazi kukumbatia tamaduni ya kutoa damu kwa hiari.
Naibu Mwenyekiti wa Shirika hilo Bi Khadija Bakaldy amesema ni jukumu la Wakaazi wa eneo la Pwani kujizatiti na kutoa damu kwa hiari mara kwa mara ili kuokoa maisha ya wagonjwa hospitalini hasa kunapotokea dharura.