Picha kwa hisani –
Wakaazi katika Kaunti ya Mombasa na kwengineko pwani wamehimizwa kujitenga na siasa ya kuhongwa fedha ili kuwaunga mkono baadhi ya viongozi.
Mwanaharakati wa kisiasa na Kiongozi wa Vijana katika eneo la Tononoka Kaunti ya Mombasa Ibrahim Jey amesema Wakaazi wa Kaunti hiyo wameshindwa kuwapata viongozi waadilifu kutokana na siasa hiyo ya ushawishi wa kifedha.
Akizungumza huko Tononoka Kaunti ya Mombasa hapo jana, Ibrahim amesema bila ya wakaazi kubadilika na kuwaweka mamlakani Viongozi waadilifu, watasalia na changamoto zao za kimaendeleo maishani.
Jey amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo kushirikiana na wanasiasa waliyo na maono na sera za maendeleo.