Mchanganuzi wa maswala ya kisiasa kaunti ya Mombasa Ali Mwatsahu amesema kuwa Ukanda wa Pwani utaimarika kimaendeleo ikiwa wakaazi wataunga mkono viongozi wenye nia ya kuboresha uongozi.
Akiongea mjini Mombasa Mwatsahu amesema kuwa ukosefu wa ushirikiano baina ya viongozi na wakaazi umepelekea eneo hili kushuhudia uongozi duni.
Mwatsahu hata hivyo amewapongeza gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho na mwenzake wa Kilifi Amason Kingi kwa juhudi zao kuwaleta pamoja viongozi mbali mbali pwani kwa lengo la kuliboresha eneo hili kisiasa na kimaendeleo.
Mchanganuzi huyo wa masuala ya kisiasa anawahimiza viongozi pwani kujitenga na mizozo ya kisiasa na badala yake washirikiane kufanikisha uongozi na maendeleo.
Taarifa na Hussein Mdune.