Picha kwa hisani –
Wizara ya elimu nchini imetangaza kwamba shule za humu nchini zitafunguliwa rasmi tarehe 4 mwezi januari mwaka ujao kwa muhula wa pili kwa wanafunzi wote wa humu nchini.
Waziri wa elimu nchini Prof George Magoha amesema muhula huo wa pili utakamilika tarehe 19 ya mezi machi ambapo wanafunzi watapewa likizo ili kutoa nafasi kwa mitihani ya kitaifa ya KCPE na KCSE itakayoanza tarehe 22 ya mwezi huo wa machi.
Akizungumza katika makao makuu ya taasisi ya mtaala KICD,baada ya kukutana na wadau wa elimu nchini Magoha amesema wanafunzi wa gredi ya nne na wale wanaopaswa kujiunga na kidato cha kwanza watasalia nyumbani huku wenzao wakikamilisha muhula wa tatu.
Kwa upande wake afisa mkuu mtendaji wa tume ya kuajiri waalimu nchini TSC Nancy Macharia amewataka walimu waliona na umri wa miaka 58 na zaidi na wale waliona matatizo ya kiafya kufanya kazi wakiwa nyumbani na kuondoa dhana kwamba wataachishwa kazi wakisalia nyumbani kwa mda mrefu.