picha kwa hisani –
Rais Uhuru Kenyatta ametuma ujumbe wa pongezi na kumtakia heri njema Rais mteule Joseph Robinette Biden, kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi uliokamilika hivi majuzi wa Marekani.
Rais Kenyatta aliutaja ushindi huo mkubwa kwenye uchaguzi huo wenye ushindani mkali, kuwa ishara ya imani waliyo nayo raia wa marekani katika uongozi wa Makamu huyo wa Rais wa zamani.
Wamarekani wameongea kwa sauti kubwa na bayana kupitia kura zao kwa kuchagua kiongozi mwenye uzoevu mkubwa, mwenye hadhi kuu na ambaye amehudumu kwa muda mrefu kuwa Rais wa Marekani.
Rais Kenyatta alisema Rais mteule Joseph Biden ni rafiki wa Kenya ambaye ziara yake ya mwisho humu nchini akiwa makamu wa Rais chini ya utawala wa Rais Barack Obama ilisaidia kufufua uhusiano kati ya Kenya na Marekani.