Story by Mwanaamina Fakii-
Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Steve Ambrose Oloo amewataka maafisa wa usalama katika eneo bunge la Kinango kushirikiana ili kutatua mizozo inayoshuhudiwa kati ya wakulima na wafugaji.
Kulingana na Oloo, hivi karibu katika eneo la Silaloni ngamia wawili waliibiwa katika eneo hilo na kuchinjwa na baadaye nyama kugawanyiwa wanajiji.
Oloo amewaonya wakaazi dhidi ya tabia hiyo huku akiwataka maafisa tawala katika eneo hilo ikiwemo machifu na manaibu wako kuwachukulia hatua kali wanaoendeleza uhalifu huo.
Kamanda huyo wa polisi amesema ni sharti maafisa wa usalama wewe katika mstari wa mbele kukabiliana na visa vya uhalifu ikiwemo kuwakamata watekelezaji wa visa.