Story by Our Correspondents-
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Taita taveta wamewaonya wanasiasa dhidi ya kufanya kampeni za mabishano na kuwateka kujitenga na tabia hiyo ili kuzuia kushuhudiwa kwa siasa za vurugu.
Kamanda wa polisi mjini Voi Bernastein Shari amewataka wanasiasa kuzingatia kalenda za mikutano yao ya kisiasa walizotoa kwa idara ya usalama ili kuepuka kuzozania sehemu za mikutano ya kisiasa na wagombea wenza au wapinzani wao wa kisiasa.
Shari amesema idara ya usalama iko tayari kuhakikisha usalama wa kaunti hiyo unaimarishwa ili kuhakikisha wakaazi wa Voi na viunga vyake wanaishi kwa amani.