Story by Charo Banda –
Kamanda wa polisi katika eneo la Malindi John Kemboi, amewaonya wakaazi wa eneo hilo dhidi ya tabia ya kupuuza masharti ya kujikinga na msambao wa Corona.
Kulinagana na Kemboi, wakaazi wengi mjini wa Malindi wamekosa kuzingatia kanuni hizo na kukosa kuvaa barakoa na kujiweka katika hatari ya kupata maambukizi.
Akizungumza na Wanahabari mjini Malindi, Kemboi ameweka wazi kwamba maafisa wa usalama watazindua msako mkali katika mji wa Malindi na yeyote atakayepatikana akikosa kuzingatia masharti hayo ataadhibiwa.
Wakati uo huo amewataka wakaazi ambao hawajapata chanjo ya kudhibiti virusi vya Corona kuvitembelea vituo vya afya ili kupokea chanjo hiyo.