Story by Our Correspondents –
Washukiwa watano wa uhalifu wametiwa nguvuni na maafisa wa polisi kwa madai ya kuhusika na tukio la uvamizi wa kigaidi katika kijiji cha Widhu eneo la Majembeni kaunti ya Lamu ambapo watu sita waliripotiwa kuuwawa.
Msemaji wa Polisi nchini Bruno Shioso amesema washukiwa hao wataendelea kuhojiwa na maafisa wa idara ya upelelezi kama uvamizi huo unahusiana na mzozo wa ardhi.
Shioso amedokeza kwamba maafisa wa usalama wanaendeleza uchunguzi kubaini iwapo tukio hilo la siku ya Jumatatu kama pia linahusiana na shambulizi ya kigaidi kwani washukiwa wote waliotiwa nguvuni na raia wa Kenya.
Hata hivyo mapema siku ya Jumanne mtu mmoja wameripotiwa kuuwawa na kisha mwili wake ukachomwa baada ya shambulizi la kivamizi kutekelezwa na Wanamgambo wa Alshabab katika eneo la Bobo-Hindi kaunti ya Lamu.