Vijana wanne wanazuiliwa na maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Likoni baada ya kunaswa na vifurushi 21 vya dawa za kulevya aina ya Cocaine katika eneo la Shika Adabu eneo bunge la Likoni kaunti ya Mombasa.
Afisa mkuu wa polisi wa eneo la Likoni Benjamin Rotich amesema wanne hao kwa majina Omar Khamis, Mwingi Khamis Mwashirika, Ahmed Ali Ahmed na Mohammed Hussein wametiwa nguvuni katika nyumba moja eneo hilo la Shika Adabu.
Rotich, anasema ulanguzi na utumizi wa dawa za kulevya katika gatuzi dogo la Likoni umeshamiri na kufichua kuwa msako dhiidi ya biashara hiyo huo utaimarishwa ili kuwanasa wahusika wote.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni