Story by Gabriel Mwaganjoni-
Maafisa wa polisi katika eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa wanamzuilia mwanamume mmoja aliyemkata panga mkewe na kuua usiku wa kuamkia siku ya Ijumaa.
Kulingana na Afisa mkuu wa polisi eneo la Changamwe David Mathiu, wawili hao walikuwa na mzozano wa nyumbani katika mtaa wa Mwagosi kabla ya mwanamume huo akamkata panga mkewe kichwani na mkononi na kumuua papo hapo na kisha akatoroka.
Japo majirani wamefika katika nyumba hiyo ili kutuliza hali, tayari mwanamke huyo alikuwa amefariki huku mwanawe mchanga wa umri wa miezi mitatu akiwa kando ya mwili wa mamake akiwa salama.
Mathiu amesema tayari wamefaulu kumtia nguvuni mwanamume huyo na wanamzuilia katika kituo cha polisi cha Changamwe huku mwili wa mkewe ukipelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani.
Uchunguzi umeidhinishwa kuhusiana na tukio hilo.