Story by Ephie Harusi –
Idara ya usalama kaunti ya Kilifi imeanzisha uchunguzi kubaini chanzo cha moto ambao ulisababisha mali ya thamani kuteketea katika shule ya upili ya Chumani.
Kamishna wa kaunti hiyo Kutswa Olaka amesema bweni la wavulana lenye idadi ya wanafunzi 124 ndilo lililoteketea wakati wanafunzi walipokuwa darasani.
Akizingumza na Wanahabari alipozuru shule hiyo, Kamishna huyo amesema mikakati tayari imeidhinishwa wanafunzi watalala katika madarasa mapya hadi ukarabati wa bweni hilo utakapokamilika.
Naye Mwakilishi wadi ya Matsangoni katika kaunti hiyo Hassan Mohamed amelaani vikali tukio hilo, akitaka uchunguzi wa haraka kuidhinishwa ili kubaini sababu zilizochangia bweni hilo kuchomeka.