Story by Mwahoka Mtsumi –
Maafisa wa Polisi wamewauwa kwa kuwapiga risasi washukiwa wawili wa uhalifu ambao walikuwa wamepanga njama ya kutekeleza uhalifu katika stage ya Ukunda kaunti ya Kwale.
Idara ya upelelezi wa jinai nchini DCI, amesema watu hao walikuwa wamejihami kwa mapanga, visu, bastola na silaha zengine hatari, wameuwawa kwa kupigwa risasi na maafisa wa polisi waliokuwa wakishika doria.
Polisi wamesema tayari usalama umeimarishwa katika kaunti nzima ya Kwale ili kuhakikisha wananchi wako salama huku wakiwataka wananchi kuripoti kwa maafisa wa usalama njama zote za kihalifu.
Akithibitisha tukio hilo, Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Ambrose Oloo amesema wakati wa tukio hilo polisi wamenasa simu za rununu, mapanga, visu na silaha zengine hatari huku polisi wakiendeleza doria.
Miili ya watu hao imepelekwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Kwale, huku polisi wakiendelea kuwasaka wahalifu wengine.