shukiwa
Story by Salim Mwakazi-
Maafisa wa polisi katika eneo la Matuga kaunti ya Kwale wamewatia nguvuni washukiwa wawili wa uhalifu katika eneo la Mbweka wadi ya Waa.
Naibu Kamishna wa gatuzi dogo la Matuga Lucy Ndemo amesema washukiwa hao wamekamatwa na sihala hatari ikiwemo vifaa butu, simu za rununu, pesa za kigeni, vazi la askari na bangi inayokisiwa kuwa ya thamani ya shilingi elfu 30.
Akizungumza na Wanahabari katika kituo cha polisi cha Kombani, Lucy amesema kutiwa nguvuni kwa wahalifu hao kumetokana na ushirikiano wa jamii na lazima watafikishwa Mahakamani.
Wakati uo huo amewataka wakaazi kuzidi kushirikiana na maafisa wa polisi katika kuimarisha usalama sawa na kuwafichua wahalifu wote kwa polisi ili watiwe nguvuni.