Story by Gabriel Mwaganjoni –
Maafisa wa polisi katika eneo la Changamwe wanawazuilia watu wanane waliotiwa nguvuni kwa kushiriki uhalifu.
Afisa mkuu wa polisi eneo hilo David Mathiu amesema wanane hao ni pamoja na wanawake wawili na wanaume sita wanaoaminika kupanga na kutekeleza uhalifu katika mitaa ya Mwagosi, Bomu, Magongo, Chaani, Portreitz miongoni mwa maeneo mengine ya gatuzi hilo dogo la Changamwe.
Wanane hao wamenaswa kwenye nyumba moja katika mtaa wa Mwagosi baada ya wakaazi kulalamikia kukithiri kwa visa vya wizi katika eneo hilo.
Wanane hao watasalia katika kituo cha polisi cha Changmwe hadi siku ya Jumatatu juma lijalo watakapofikishwa Mahakamani.