Story by Janet Shume –
Maafisa wa idara ya upelelezi wa jinai wamemuua kwa kumpiga risasi mshukiwa mmoja wa ujambazi katika eneo la Kiteje kaunti ya Kwale.
Kamanda mkuu wa polisi kaunti ya Kwale Ambrose Oloo amesema majambazi wengine wawili wametoroka na majeraha ya risasi na akawataka wakaazi kutowaficha wahalifu.
Oloo amesema maafisa wa polisi wamefanikiwa kunasa bunduki moja aina ya Ak47 pamoja na risasi na vifaa vya kutengeza vilipuzi katika operesheni hiyo ya kumaliza ugaidi inayoendelezwa katika kaunti ya Kwale.
Wakati uo huo amewasihi wakaazi kushirikiana na maafisa wa polisi katika kuimarisha usalama mashinani.