Maafisa wa Polisi mjini Malindi wamenasa takriban misokoto 550 ya bangi yenye thamani ya shilingi elfu 120 katikati mwa mji wa Malindi.
Kamanda wa polisi mjini Malindi John Kemboi, amesema maafisa wa upelelezi walipata taarifa kutoka kwa mmoja wa makachero wao kabla ya kumkamata jamaa aliyekuwa anasafirisha bangi hiyo kwa pikipiki.
Kemboi amesema kwa sasa wanaendeleza uchunguzi kubaini mmiliki wa bangi hiyo huku jamaa huyo aliyekamatwa akiendelea kuzuliwa na maafisa wa polisi kuhojiwa.
Kemboi ametoa onyo kali kwa wananchi, akisema watahakikisha biashara hiyo haramu ya walanguzi wa dawa za kulevya inasitishwa mjini Malindi.