Picha kwa Hisani –
Maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi nchini ATPU, wamemuuwa kwa kumpiga rasasi mshukiwa mmoja wa ugaidi huku wengine wakifanikiwa kutoroka na majeruhi ya risasi.
Maafisa hao walivamia maficho ya mashukiwa hao wa ugaidi katika eneo la Tiribe kaunti ya Kwale hali iliopelekea kushuhudiwa kwa makabiliano makili ya risasi na kumuuwa Juma Athman Mwengo.
Akithibitisha tukio hilo, Afisa mkuu wa Polisi eneo la Matuga Francis Nguli amesema washukiwa hao walikuwa wanapenga kutekeleza mashambulizi ya kigaidi katika eneo la Mombasa na Kwale na juhudi zao zinazimwa na polisi.
Hata polisi wamesema msako mkali wa kuwasaka washukiwa wa ugaidi waliofanikiwa kutoroka unaendelea ili kuhakikisha usalama wa wananchi wa kaunti ya Kwale unalindwa.
Hata hivyo Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Kwale.