Story by Janet Shume-
Maafisa wa polisi kaunti ya Kwale wanamzuilia kijana mmoja kwa jina Hamisi Jira aliyepatikana akisafirisha kwa pikipiki vyuma vya mifereji ya maji vilivyong’olewa kutoka kwa mradi wa maji wa serikali.
Polisi wamesema Hamis ametiwa nguvu katika wadi ya Puma eneo bunge la Kinango akiwa na mwenzake aliyefanikiwa kutoroka.
Afisa mkuu wa usalama eneo hilo Selina Kiluga amesema tayari uchunguzi umeidhinishwa wa kumsaka kijana aliyetoweka wakati wa oparesheni hiyo.
Aidha amewahimiza wakaazi kushirikiana na maafisa wa usalama kuripoti visa vyovyote vya kihalifu ikiwemo vya uharibifu na wizi wa mabomba na vyuma vya maji ili wahusika wachukuliwe hatua.