Story by Gabriel Mwaganjoni
Maafisa wa polisi katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa wanamzuilia mshukiwa mmoja wa ujambazi waliyemtia nguvuni.
Greggory Isaac Amimu amenaswa na Maafisa wa polisi waliyokuwa wakimsaka kwa muda kutokana na kuhusishwa na misururu ya uhalifu katika gatuzi dogo la Likoni.
Kulingana na polisi, Amimu amekuwa akijificha katika mapango tofauti kwenye fukwe za bahari hindi na amekuwa akihusishwa na visa vya uhalifu katika eneo la Likoni sawa na kuongoza kundi la majambazi wanaojihami kwa visu na mapanga.
Hata hivyo ametajwa kuliongoza kundi linalofahamika kama Panga Boys na anaendelea kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Likoni akisubiri kufikishwa Mahakamani.