Story by Gabriel Mwaganjoni –
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amesema walimu wanaotumwa katika kaunti ya Lamu ili kufanya kazi wamehakikishiwa usalama wao.
Elungata amesem Serikali imeimarisha usalama katika kaunti nzima ya Lamu na hasa katika maeneo ya msitu wa Boni ambayo yameathirika pakubwa na msukosuko wa usalama.
Akizungumza huko Mokowe katika kaunti hiyo wakati wa ziara yake ya kiusalama, Elungata amesema vitengo vya usalama vimeliwajibikia barabara swala la usalama wa kaunti ya Lamu, huku akiwataka walimu na wakaazi wa kaunti hiyo kutohofia lolote.
Hata hivyo, Elungata amewahimiza wakaazi wa kaunti hiyo kuripoti matukio au njama zozote zinazoweza kuvuruga usalama wa kaunti hiyo ili wahusika wakabiliwe kisheria.