Story by Gabriel Mwaganjoni
Maafisa wa polisi katika kaunti ya Mombasa wameidhinisha uchunguzi kuhusu kifo cha mwanamume mmoja katika mtaa wa Kiziwi eneo la Tudor Kisiwani Mombasa.
Mwanamume huyo aliyetambulika kama mfanyabiashara, anadaiwa kupigwa risasi mara kadhaa na kuuliwa ndani ya gari lake pambizoni mwa maziara ya manyimbo eneo hilo la Tudor.
Polisi hata hivyo walifika mahali hapo na kuuchukua mwili wa jamaa huyo na kuupeleka katika hifadhi ya maiti ya hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani.
Hakuna taarifa zaidi iliyotolewa na maafisa wa polisi kuhusiana natukio hilo japo tayari uchunguzi umeidhinishwa ili kubaini kiini cha tukio hilo.