Story by Bakari Ali –
Mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya Pwani John Elungata amekana madai ambayo yamekuwa yakienezwa kwamba maafisa wa usalama katika ukanda wa pwani wanahusika na ongezeko la visa vya watu kupotea katika hali tata.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Elungata amesema licha ya visa hivyo kukithiri maafisa wa usalama hawajahusika kwa njia yoyote ile na matukio hayo huku akidai kwamba idara hiyo inatekeleza kazi yake kisheria.
Elungata amesema idara ya usalama nchini imeweka mikakati mwafaka ya kufanya uchunguzi dhidi ya visa hivyo na kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena humu nchini.