Afisa wa maswala ya Jinsia na haki za watoto katika Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu nchini la MUHURI Bi Topista Juma amewataka maafisa wa polisi kuitekeleza misako yao kwa kuzingatia utu na haki za kibinadamu.
Bi Topista amesema kwamba mara nyingi misako hiyo huwa na athari ya muda mrefu kwa maisha ya wanawake na watoto wanaojipata katikati ya vita hivyo dhidi ya ugaidi hapa Pwani.
Bi Topista hata hivyo ametaka kuwe na mwafaka kuhusiana na swala hilo la ugaidi na Serikali kuu kuwa wazi kuhusiana na kuwabadili vijana waliyosajiliwa ili kupata mafunzo ya kigaidi na baadaye kurudi kisiri nchini.
Kulingana na Afisa huyo wa Jinsia na haki za watoto Pwani, tayari Shirika hilo la MUHURI linaendeleza hamasa kwa maafisa wa polisi na jamii yenyewe ya Pwani kuhusiana na swala hilo la ugaidi na jinsi polisi wanavyoweza kufanya kazi na jamii katika kulidhibiti.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.