Mwakilishi wa wadi ya Mikindani Juma Renson Thoya anataka maafisa wa usalama kupewa mafunzo ya huduma ya kwanza, ili waweze kuokoa maisha pindi kunapotokea dharura.
Thoya ameeleza kuwa iwapo maafisa hao watakua na ufahamu wa mbinu za kutoa huduma ya kwanza watakuwa na uwezo wa kutoa usaidizi wa kwanza wa kuokoa maisha kunapotokea mikasa ya aina yeyote.
Thoya amesema haya wakati wa kikao cha kutoa hamasa kuhusu huduma ya kwanza kwa jumla ya maafisa tawala 50 kilichoandaliwa jijini Mombasa.
Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.