Maafisa wawili wa polisi wameripotiwa kufariki dunia huku watu wengine 10 wakijeruhiwa vibaya baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani.
Kulingana na walioshuhudia tukio hilo, maafisa hao wa polisi walikuwa wamemkamata dereva wa tuktuk na kuanza kuendesha tuktuk hiyo ndio akapoteza mwelekeo na kugongana ana kwa ana na matatu ya abiria.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa polisi kaunti ya Kwale Tom Odero ametofautiana na taarifa hiyo na kusema kuwa idara ya polisi itatoa taarifa kamili baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa ajali hiyo.
Odero amesema waliojeruhiwa kwenye ajaili hiyo wamekimbizwa katika zahanati ya Waa huku wengine wakikimbizwa katika hospitali ya Kwale kwa matibabu ya dharura.
Miili ya maafisa hao wawili wa polisi walioaga dunia inahifadhiwa katika hospitali kuu ya ukanda wa Pwani.
Taarifa na Michael Otieno na Salim Mwakazi.