Picha kwa hisani –
Maafisa wa polisi katika eneo la Changamwe kaunti ya Mombasa wanamsaka mtu moja aliyewapiga risasi watu watatu na kuwauwa.
Kamanda mkuu wa polisi gatuzi dogo la Changamwe David Matthew amesema watu wanne walikuwa kwenye gari dogo lililokuwa likielekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi eneo la Changamwe kabla ya tukio hilo.
Matthew amesema gari lingine dogo ambalo idadi ya watu waliyokuwamo ndani ya gari hilo haijabainika lililokuwa likitoka upande wa pili yamepishana na dereva wa gari moja akachomoa bastola na kuwapiga risasi wenzake na kumuuwa dereva papo hapo.
Watu wengine watatu walijeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali kuu ya Ukanda wa Pwani kupokea matibabu ambapo wawili wameripotiwa kufariki huku mmoja anayeendelea kupigania uhai wake katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Polisi wamekusanya jumla ya risasi 40 katika gari la wale waliyouwawa katika tukio hilo sawia na simu za rununu na stakabadhi nyinginezo zinazowasaidia katika upelelezi.
Hakuna aliyetiwa nguvuni kufikia sasa, japo polisi wameimarisha uchunguzi wao kuhusu tukio hilo.