Story by Salim Mwakazi-
Idara ya usalama kaunti ya Kwale imewahakikishia usalama wa kutosha wageni na waekezaji katika sekta ya utalii wanaolenga kuwekeza katika kaunti hiyo kama njia mojawapo ya kuboresha sekta ya utalii.
Kamishna wa kaunti hiyo Gideon Oyagi amesema eneo la Diani linatarajiwa kurekodi idadi kubwa ya watalii kuanzia mwezi huu wa Novemba huku akihoji kwamba kwa ushirikiano na wadau wa utalii mikakati mwafaka imewekezwa.
Akizungumza na Wanahabari, Oyagi ametoa tahadhari kwa wageni wanaolenga kujivinjari katika fuo za bahari hindi kuwa waangalifu sawa na kuzingatia taratibu zilizopo ili kupuka majanga.