Idara ya usalama huko Malindi kaunti ya Kilifi imesitisha doria katika eneo la Kwa Chocha, kutokana na madai kwamba mafisa wa polisi wanahangaisha waakazi wakati wa doria hizo.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama eneo la Malindi Karung’o Kamau amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa baada ya wakaazi wa eneo hilo kuandamana kulalamikia kuhangaishwa na maafisa wa polisi.
Kamau vile vile amesema kuwa wadau wa usalama katika eneo hilo wanapania kufanya mkao juma lijalo kujadiliana na kuibuka na mbinu muafaka za kuimarisha usalama wa wakaazi wa eneo hilo.
Taarifa Esther Mwagandi.