Story by: Gabriel Mwaganjoni
Maafisa wa polisi kaunti ya Mombasa wamemtia nguvuni jamaa mmoja aliyesababisha ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha Polisi wa trafiki alipokuwa kazini katika daraja la Nyali kwenye barabara kuu ya Mombasa–Malindi.
Polisi wamesema marehemu Julius Marwa akiwa kazini alisimamisha gari moja ili kulikagua hatua iliyomkera dereva wa gari hilo Osman Jama Abdi na kusababisha polisi huyo kuufungua mlango wa gari hilo ili kulizima ndipo Abdi alipoliondoa gari hilo kwa kasi huku polisi huyo akining’inia kabla ya kuanguka na kuganyagwa na gari hilo.
Afisa mkuu wa polisi wa kituo cha Urban Maxwell Agoro amesema Marwa aliyekuwa akihudumu katika kituo cha polisi cha Makupa ameuaga dunia baada ya kukimbizwa katika hospitali ya Joacham eneo la Kengeleni.
Kwa sasa Abdi anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Makupa huku gari lake likizuiliwa kituoni humo akisuburi kufikishwa mahakamani punde tu uchunguzi utakapokamilika.