Kamati ya nidhamu ya Chama cha Amani National Congress ANC, imemtimua chamani Seneta wa Kakamega Cleophas Malala.
Katika mkutano wa Baraza kuu la kitaifa la Chama hicho uliyoongozwa na Wakili wa chama hicho Profesa Mukhwana Alutalala amesema wanachama hao wameafikia kumuondoa chamani Malala baada ya kuonekana kuunga mkono Chama cha ODM katika uchaguzi mdogo wa eneo bunge la Kibra mwaka wa 2019.
Alutalala amesema licha ya Malala kuagizwa kufika mbele ya Baraza kuu la chama hicho ili kujieleza ni kwa nini hafai kutimuliwa chamani, Seneta hiyo alikaidi agizo hilo.
Kwa upande wake Kinara wa Chama hicho Musalia Mudavadi, ameshikilia kuwa ni sharti kwa sheria za chama hicho kufuatwa kikamilifu na kila kiongozi sawia na wafuasi wa chama hicho.