Mtu mmoja anahofiwa kufariki baada ya jumba la ghorofa 8 kuanguka huko Malindi kaunti ya Kilifi.
Kulingana na baadhi ya wakazi walioshughudia kuanguka kwa jumba hilo, mkasa huo ulitokea alfajiri baada ya kusikika kwa mlipuko mkubwa. Nyumba hiyo inadaiwa imeanguka kutokana na mvua kubwa inayoshughudiwa katika eneo hilo.
Kwa mjibu wa mshirikishi wa shirika la msalaba mwekundu kanda ya Pwani, Hassan Musa amesema kuwa juhudi za ukozi zinaendelea huku tayari watu 8 wakiwa wameokolewa.
Shughuli za uokozi zikiendelea katika jumba liloanguka Malindi. Picha/ Charo Banda
Muonekano wa jengo liloanguka kabla ya mkasa. Picha/ Charo Banda
Muonekano wa jumba baada ya kuanguka mapema leo mjini Malindi katika mkasa wa leo. Picha/ Charo Banda.
Gari liloangukiwa na kuta za jumba liloanguka Malindi. Picha/ Charo Banda
Maofisaa wa uokozi kutoka msalaba mwekundu na KDF wakiwashughulikia wahanga wa mkasa wa kuanguka kwa jumba mjini Malindi. Picha/ Charo Banda