Story by Janet Shume-
Chama cha maafisa wa polisi waliostaafu nchini NAPOK kimesema visa vya matatizo ya afya ya kiakili vinavyoshuhudiwa miongoni mwa maafisa wa polisi baada ya kustaafu kwa sasa vimepungua.
Kulingana na Phedilia Kisinyo mmoja wa mwanachama katika chama hicho, hatua hiyo imechangiwa na ushirikiano kati yao na kuidhinishwa kwa chama hicho kwa minajili ya kuendeleza umoja kati yao hata baada ya kustaafu.
Kisinyo amesema ushirikiano uliopo kati yao na maafisa waliopo kazini umechangia pakubwa kwa maafisa waliostaafu kujiendeleza kimaendeleo bila ya changamoto.
Wakati uo huo amesema mikakati ya kutembeleana kwa maafisa hao katika makaazi yao iliyoidhinishwa na chama hicho kimewasaidia pakubwa maafisa waliostaafu kuondoa upweke na kuimarisha afya yao ya kiakili.