Story by Mercy Tumaini –
Mbunge wa Kilifi kusini Ken Chonga amewataka wakaazi wa Chonyi na Pwani kwa ujumla kuwaheshimu wazee wa kaya
Akizunguza wakati wa halfa ya kuapishwa rasmi kwa Mwenyekiti wa mpya wa Baraza la jamii ya wachonyi katika eneo la mwembe kati kaunti ya Kilifi, Chonga amesema wazee wamekuwa wakikosewa heshima kutokana na ubinafsi wa viongozi katika eneo hilo.
Chonga amesema wazee wanamchango mkubwa katika jamii hasa katika kutatua maswala mbalimbali ikiwemo ya kifamilia na baadhi ya mizozo ya mashamba.
Kwa upande wake Mwenyekiti mpya wa Baraza hilo Mwalimu Patrick Rasi amesema kuna haja ya wakaazi katika eneo zima la pwani kuhakikisha wanamuunga mkono katika jukumu alililopewa ili wanufaike kimaendeleo.
RASI – KUUNGWA MKONO 01 12 21
Hata hivyo shughuli za kuapishwa kwa mwenyekiti wa baraza hilo zimehudhuriwa na Balozi Sophy Kombe, Mwansiasa Ben Kai miongoni mwa viongozi wengine.