Story by Hussein Mdune
Mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Taita taveta Patience Nyange amemteuwa Dalton Mwaghogho kama mgombea mwenza wake kwenye uchaguzi mkuu wa Agosti tarehe 9
Akizungumza katika halfa iliyoandaliwa mjini Voi, Patience amesema amemchagua Dalton kutokana na tajriba yake kwenye maswala ya Uhasibu huku akihoji kwamba atasaidia pakubwa katika kuinua maisha ya wakaazi wa kaunti hiyo.
Patience hata hivyo amesema wakati ni sasa kwa wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta kuwachagua viongozi kwa kuzingatia sera zao na wala sio vyama vya kisiasa huku akiwataka kujitenga na viongozi wachochozi.
Kwa upande wake Dalton Mwaghogho ambaye aliwahi kuhudumu kama Mhasibu katika chuo kikuu cha Taita taveta na pia chuo cha TUM mjini Mombasa ameahidi kushirikiana Patience katika kuboresha maisha ya wakaazi wa kaunti hiyo.