Mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amelitaka Bunge la kaunti ya Kilifi kupitisha mswada wa kupiga marufuku usafirishaji wa malighafi katika kaunti hiyo.
Akizungumza na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya kaunti hiyo, Owen amesema usafirishaji wa malighafi hususan madini na matunda kutoka kaunti ya Kilifi hadi kaunti zingine umewanyima vijana wengi nafasi za ajira.
Owen amekariri kuwa endapo serikali ya kaunti hiyo itaekeza zaidi katika ujenzi wa viwanda vya kutengeneza bidhaa hizo basi tatizo la uhaba wa ajira litatuliwa.
Mbunge huyo amedokeza kuwa kaunti ya Kilifi inajulikana sana kwa kuwa na malighafi kwa wingi ikiwemo madini, nazi na matunda lakini hakuna kiwanda hata kimoja cha kutengeneza bidhaa hizo.
Taarifa na Marieta Anzazi.