Picha Kwa Hisani – Otile Brown na Nabayet.
Mwanamuziki Otile Brown ametangaza rasmi kuachana na mpenzi wake wa muda mrefu kutoka Ethiopia Nabayet, kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Picha Kwa Hisani – Nabayet.
Wawili hao wamekuwa pamoja katika mahusiano ya umbali tangu mwezi Machi 2019, baada ya Otile kuachana na Vera Sidika.
Picha Kwa Hisani – Otile Brown na Nabayet.
Otile ameeleza kuwa Nabayet pia maarufu kama Nabbi, alikuwa amewasili nchini ili kuzungumza kuhusu masuala yanayowakabili, lakini haikufaulu vyema.
Picha Kwa Hisani – Otile Brown na Nabayet.
Kulingana na mwanamuziki huyo, uamuzi huo wa kuachana ulikuwa makubaliano ya pande zote mbili, na sasa yupo single tena.
Picha Kwa Hisani – Otile Brown.
“Mimi na Nabbi hatuko pamoja tena, mara ya mwisho tukiwa pamoja tulijaribu kutafuta njia ya kwenda mbele lakini tuliamua kuachana kwa bahati mbaya….yeye ni mtu wa ajabu na kwa ajili ya hayo nitamheshimu milele na hata kumjali
Namtakia mema anapoendelea na maisha yake Ubarikiwe,” Otile Aliandika.