Picha kwa hisani –
Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi amefikishwa mahakamani huko Nakuru kujibu tuhuma za kutoa matamshi yanayodaiwa kuwa ya uchochezi.
Wakili wa Sudi,Isaac Terer amesema mbunge huyo anakabiliwa na mashataka matatu ikiwemo kutoa semi za uchochezi, kuonyesha mienendo isiofaa miongoni mwa mashtaka megine.
Terer amesema mbunge huyo ambae anazuiliwa na polisi tangu alipojisalimisha hapo jana atajua iwapo ataachiliwa kwa dhamana kikao cha kusikilizwa kwa kesi yake kitakapokamilika mchana wa leo.
Haya yamejiri baada ya Sudi kujisalimisha katika kituo cha Polisi cha Nakuru Hapo jana baada ya kusakwa na polisi kwa madai ya kutoa matamshi tatanishi.