Onyo kali limetolewa kwa wale wanaonyakua maeneo yanayotumiwa na wavuvi ili kuegesha maboti yao au kuendeleza shughuli zao za uvuvi.
Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameutaja unyakuzi huo kama uliyosambaratisha shughuli za kiuchumi kwa wavuvi hao akitaja hali hiyo kukomeshwa mara moja.
Amesema ataliwasilisha swala hilo bungeni ili kuona kwamba wanyakuzi hao wanaandamwa ili kutoa nafasi kwa wavuvi kuendeleza shughuli zao bila ya kuhangaishwa na mabwenyenye hao.
Wakati uo huo, Nassir ametaka usimamizi wa bandari zote za Ukanda wa Pwani kuwa chini ya Serikali za Kaunti zinazopakana na Bahari hindi na wala sio Serikali kuu.
Nassir ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa maboti 28 kwa wavuvi wa Kaunti hiyo ya Mombasa.