Idara ya usalama kaunti ya Kwale imeonya wakaazi wa kaunti hiyo dhidi ya kuwaua wazee kwa kisingizioa cha tuhumu za uchawi.
Kamanda wa Polisi kaunti ya Kwale Joseph Nthenge amesema atakayepatikana akiendelea unyama huo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Nthenge amewataka wakaazi wa kaunti ya Kwale kushirikiana na wazee wa mtaa, machifu na vitengo vya usalama kuhakikisha haki za kibidamu zinalendwa sawia na kuwatunza wazee.
Kauli yake imejiri baada ya visa viwili vya hivi majuzi vya mauaji ambapo wazee wawili wa umri wa miaka 65 na 70 kutoka eneo la Kinango na Lunga lunga kuuwawa kwa kukatwa kinyama kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana kwa tuhuma za uchuwi.