Story by Janet Shume-
Wadau wa kimazingira katika kaunti ya Kwale wamesema utupaji taka ovyo ikiwemo vifaa vya kielektroniki na chupa za plastiki umechangia uharibifu wa mazingira pamoja na kuathiri afya ya binadamu.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mazingira nchini NEMA tawi la kaunti ya Kwale, Godfrey Wafula ameitaka jamii kutambua umuhimu na kufuata kanuni za utupaji taka hususan za kielektroniki ili kupunguza athari za kimazingira.
Wafula amesema ni lazima wananchi wawe waangalifu sawa na kuyalinda mazingira
Wafula amewataka wakaazi kushirikiana na wahusika wanaoshughulikia utupaji taka za kielektroniki ili kuzuia madini ya vyuma hivyo kuingia katika mazingira na kusababisha athari mbalimbali ikiwemo uchafuzi wa maji.