Story by: Our Correspondents
Afisa wa Mamlaka ya kukabiliana na ukame kaunti ya Tana River Kennedy Omondi amesema zaidi ya wakaazi elfu 80 katika kaunti hiyo wanahitaji msaada wa dharura wa chakula.
Kulingana na Omondi, eneo la Tana Kaskazini ndilo limeathirika zaidi na ukame na kuna haja ya hatua za dharura kuchukuliwa ili kuwanusuru wakaazi wa eneo hilo wanaokabiliwa na kiangazi kikali.
Omondi amesema wakaazi hao wanaweza kusaidika kutokana na mpango wa cash transfer, chakula ama mpango wowote utakaovunja makali ya baa la njaa.
Amebainisha kuwa uwepo wa shamba la unyunyizaji la Hola na makao makuu ya kaunti ndiyo imepelekea uwepo wa mbinu mbalimbali za kuibuka na mikakati ya kuwasaidia wahanga wa njaa.