Kampuni ya Uniliver inayotengeneza sabuni ya kufulia ya Omo kwa ushirikiano na kampuni ya usafiri ya Uber inakupa fursa ya kutenda mema mwezi huu mtukufu wa Ramadan.
Kampuni hizi mbili zinakupa fursa ya kipekee ya kupeana nguo, chakula na bidhaa zenginezo zisizoharibika kwa haraka kwa wale wasiojiweza katika jamii kupitia app ya Uber mjini Mombasa.
Shiriki katika juhudi hizi kwa:
1.Kufungua app yako ya Uber kati ya saa sita mchana na saa nane mchana (12pm – 2pm) siku ya Jumamosi ya tarehe 25 May 2019.
2. Enda kwa sehemu ya ‘UberCARE’
3. Weka sehemu ambayo upo na ungependa kufuatwa.
4. Bonyeza kitufe cha UberCARE ili kuitisha huduma ya bure ya UberCARE
5. Iwapo utafanikiwa UberCARE itafika mlangoni kwako kuchukua mchango wako. Iwapo hutafanikiwa endelea kuweka ombi lako hadi ufanikiwe.
6.Uber CARE inapokaribia toka nje ya nyumba ili iwe rahisi kwa dereva kuchukua mchango wako.