Wasanii Brown Mauzo na Ommy Dimpoz wameamua kufichua siri zao ambazo wamekuwa wakizificha kwa muda mrefu.
Kupitia kurasa zao za Instagram wawili hao wameweka bayana kuwa wapo na watoto.
Ommy Dimpoz ndiye alianza msururu huo wa kutoboa siri kwa kupachika video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anasukuma kijigari cha mtoto. Video hiyo iliambatanishwa na ujumbe uliosema:
“Vipi Dengue Imeisha Nirudi nae? Haya Nafikiri yale Maswali ya unafanya nini Ulaya kila siku YAMEISHA😁😁”
Naye Brown Mauzo alidandia msururu huo kwa kuanika mwanawe hadharani kwa mara ya kwanza. Kwenye ujumbe huo alifichua jina la mtoto huyo ambalo linaisha kwa Mauzo.
“Hakeem young king👑cc:@hakeem_mauzo
#MrLoverMan”