Mahakama ya mjini Mombasa imemhukumu mbunge wa Changamwe Omar Mwinyi kifungo cha miaka minne gerezani baada ya kupatikana na kosa la kuwajeruhi maafisa wa polisi.
Hakimu Mkuu Evans Makori ametoa uamuzi huo akisema kuwa ushahidi uliotolewa mahakamani umedhihirisha wazi kuwa Mwinyi na wafuasi wake waliwajeruhi Dennis Nambisia na Agapio Ndwiga wakati wa kura za utezi wa chama cha ODM mwaka uliopita.
Hakimu huyo ameeleza kuwa ripoti ya matibabu imeonyesha kuwa maafisa hao wa polisi walijeruhiwa vibaya kufuatia uvamizi huo.
Kabla ya kutoa uamuzi huo, vikao vya mahakama vimehairishwa kwa mda ili kutoa nafasi kwa mbunge huyo kujiandaa kutoa malilio yake baada ya upande wa mashtaka kuomba mda zaidi ili kutoa ombi kulingana na sheria.
Maafisa hao wa polisi walikuwa wakitoa ulinzi kwa wapiga kura na maafisa wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC wakati wa tukio hilo.