Picha kwa Hisani –
Wagombea kiti cha ubunge cha Msambweni walioko kwenye vyama vya kisiasa wameratibiwa kuwasilisha nakala zao za uteuzi kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC hii leo kabla kuidhinishwa kuwania kiti hicho.
Omar Boga wa chama cha ODM amekuwa wakwanza kuwasilisha stakabadhi zake na kuidhinishwa rasmi kugombea kiti hicho na alikua ameandamana na gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho ,Gavana wa tanariver Dhado Godana na seneta wa siysa James Orengo na baadhi ya wabunge.
Uchaguzi huo mdogo wa ubunge wa msambweni utaandaliwa terehe 15 mwezi disemba na umewavutia wagombea kumi na moja.