Story by Bakari Ali –
Wakenya wametahadharishwa dhidi ya kuhadaiwa na wanasiasa wakati huu ambapo taifa linaelekea katika uchaguzi mkuu ujao.
Msemaji wa Serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema ni wakati mwafaka kwa wakenya kutathmini maisha yao ya baadaye badala ya kuhadaiwa na wanasiasa wanaojali maslahi yao binafsi.
Oguna amewataka wakenya kuzingatia viongozi waadilifu kwani siasa bora ndio itakayoleta maendeleo kwa taifa hili.
Wakati uo huo amewaonya wanasiasa dhidi ya kuyatumia majukwaa ya dini katika kuendeleza siasa zao, akisema hatua hiyo haiendani na muongozi wa dini.