Story by Rasi Mangale –
Msemaji wa Serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amewahimiza vijana kuzidi kudumisha amani wakati huu ambapo taifa linajiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kukutana na makundi ya vijana katika ukumbi wa Social hall mjini Kwale, Oguna amesema vijana wanafaa kuwa makini na kujitenga na wanasiasa wasiojali malengo ya vijana.
Oguna hata hivyo amedokeza kwamba serikali ina malengo ya kununua ng’ombe 2,600 kwa wafugaji kutoka kaunti ya Kwale kwa gharama ya shilingi milioni 40 ili kuwapunguzia hasara wakulima kutokana na kiangazi kikali.
Wakati uo huo ameweka wazi kwamba Serikali inalenga kutoa msaada wa chakula kwa familia elfu 26 zilizoathirika na ukame katika kaunti ya Kwale na zitakuwa zikipokea shilingi elfu 3 kila mwezi ili kukidhi mahitaji yao hadi pale hali itakaporudi kuwa sawa.